Zaeni Matunda Mema
[1]
Zaeni matunda mema
Zaeni matunda yale
Zaeni yenye baraka,
Zaeni ya heri.
[chorus]
Bwana akiyapokea
Yatabarikiwa vyema
Zaeni matunda mema
Zaeni ya heri.
[2]
Safisha mwenendo wako
Safisha matendo yako
Safisha na BwanaYesu,
Safisha yote.
[chorus]
Bwana akiyapokea
Yatabarikiwa vyema
Zaeni matunda mema
Zaeni ya heri.
[3]
Fanyeni kazi kindugu
Fanyeni kazi kwa bidii
Fanyeni na Bwana Yesu,
Fanyeni nyote.
[chorus]
Bwana akiyapokea
Yatabarikiwa vyema
Zaeni matunda mema
Zaeni ya heri.
[4]
Tolea matunda yako
Pamoja na moyo wako
Naye Bwana Mungu,
Wako atakubariki.
[chorus]
Bwana akiyapokea
Yatabarikiwa vyema
Zaeni matunda mema
Zaeni ya heri.
[5]
Baraka za Mungu Baba
Baraka za Mungu Mwana
Na za Roho Mtakatifu,
Ziwe nanyi nyote.
[chorus]
Bwana akiyapokea
Yatabarikiwa vyema
Zaeni matunda mema
Zaeni ya heri.
Support Mysongbooks
Support us by joining the Buy Me A Coffee community and making a small donation, you can help us expand our library and ensure that music lovers everywhere can enjoy their favorite songs to the fullest. We're passionate about music, and we know you are too, so let's work together to keep the music alive.
Thank you for being a part of our community and supporting our mission to provide the best lyrics library on the internet.