Twonane Milele
[1]
Nyimbo na tuziimbe tena
Za alivyotupenda mbele
kwa damu ya dhamani sana
Mbinguni kwonana milele
[chorus]
Twonane milele, twonane bandarini kule X2
[2]
Hupozwa kila aoshwaye
Kwa damu ya kondoo yule
Ataishi afurahiye
Vya Yesu Mbinguni milele
[chorus]
Twonane milele, twonane bandarini kule X2
[3]
Hata sasa hufurahia
Tamu yake mapenzi yale
Je, kwake tukifikilia
Kutofarakana milele?
[chorus]
Twonane milele, twonane bandarini kule X2
[4]
Twende mbele kwa jina lake
Hata aje Mwokozi yule
Atatukaribisha kwake
Tutawale naye milele
[chorus]
Twonane milele, twonane bandarini kule X2
[5]
Sauti zetu tuinue
Kumsifu Mwokozi yule
Ili watu wote wajue
Wokovu u kwake milele
[chorus]
Twonane milele, twonane bandarini kule X2
Support Mysongbooks
Support us by joining the Buy Me A Coffee community and making a small donation, you can help us expand our library and ensure that music lovers everywhere can enjoy their favorite songs to the fullest. We're passionate about music, and we know you are too, so let's work together to keep the music alive.
Thank you for being a part of our community and supporting our mission to provide the best lyrics library on the internet.