Jiwe Kuu La Pembeni
[1]
Mungu ni Baba wetu
Ndiye Muumba vyote
Uwezo na ushindi
Hupatikana kwake.
[chorus]
Bwana Mungu asema
Tazama naliweka
Jiwe kuu la pembeni
Lililo jaribiwa
[2]
Bwana wetu ni Kristo
Ndiye mwamba wa pekee
Jiwe kuu la pembeni
Liliwekwa na Mungu
[chorus]
Bwana Mungu asema
Tazama naliweka
Jiwe kuu la pembeni
Lililo jaribiwa
[3]
Yesu alilijenga
Kanisa juu ya mwamba
Milango ya kuzimu
Haiwezi kushinda.
[chorus]
Bwana Mungu asema
Tazama naliweka
Jiwe kuu la pembeni
Lililo jaribiwa
[4]
Naye Yesu ni kichwa
Ni kichwa cha kanisa
Naye ni mzaliwa
Wa kwanza toka wafu
[chorus]
Bwana Mungu asema
Tazama naliweka
Jiwe kuu la pembeni
Lililo jaribiwa
[5]
Mungu Baba atukuzwe
Baba na Bwana Yesu
Aliyetubariki
Baraka za rohoni.
[chorus]
Bwana Mungu asema
Tazama naliweka
Jiwe kuu la pembeni
Lililo jaribiwa
Support Mysongbooks
Support us by joining the Buy Me A Coffee community and making a small donation, you can help us expand our library and ensure that music lovers everywhere can enjoy their favorite songs to the fullest. We're passionate about music, and we know you are too, so let's work together to keep the music alive.
Thank you for being a part of our community and supporting our mission to provide the best lyrics library on the internet.