Eneza Habari
[1]
Eneza habari humu duniani
Popote panapo moyo wa huzuni,
Ndimi za Wakristo zitangaze neno,
Yupo mfariji
[chorus]
Yupo mfariji yupo mfariji
Roho mtakatifu ndiye msaidizi
Eneza habari humu duniani
Yupo mfariji
[2]
Mfalme wa wafalme, Yesu, umtazame
Ametuletea sifa ya milele
Mateka wapate ukombozi wake,
Yupo mfariji
[chorus]
Yupo mfariji yupo mfariji
Roho mtakatifu ndiye msaidizi
Eneza habari humu duniani
Yupo mfariji
[3]
Niwezeje mimi kutamka vizuri
Kumsifu mwokozi aliye mbinguni?
Nitangaze sasa, neno la furaha,
Yupo mfariji.
[chorus]
Yupo mfariji yupo mfariji
Roho mtakatifu ndiye msaidizi
Eneza habari humu duniani
Yupo mfariji
[4]
Wenzangu tuimbe nyimbo za milele
Mbinguni tujaze na shukrani tele
Upendo wa Bwana ujulike sana.
Yupo mfariji
[chorus]
Yupo mfariji yupo mfariji
Roho mtakatifu ndiye msaidizi
Eneza habari humu duniani
Yupo mfariji
Support Mysongbooks
Support us by joining the Buy Me A Coffee community and making a small donation, you can help us expand our library and ensure that music lovers everywhere can enjoy their favorite songs to the fullest. We're passionate about music, and we know you are too, so let's work together to keep the music alive.
Thank you for being a part of our community and supporting our mission to provide the best lyrics library on the internet.