Baba Yetu Aliye Mbinguni
[1]
Baba yetu aliye mbinguni
Amenifurahisha yakini
Kuniambia mwake chuoni
Ya kuwa nami Yesu pendoni
[chorus]
Anipenda Mwokozi Yesu
Anipenda, anipenda
Anipenda Mwokozi Yesu
Anipenda mimi
[2]
Nimwachapo kutanga mbali
Yeye yu vivyo hupenda kweli
Hunirejeza kwake moyoni
Kweli yu nami Yesu pendoni
[chorus]
Anipenda Mwokozi Yesu
Anipenda, anipenda
Anipenda Mwokozi Yesu
Anipenda mimi
[3]
Anipenda! nami nampenda
Kwa wokovu alionitenda
Akanifia msalabani
Kwa kua nami Yesu pendoni
[chorus]
Anipenda Mwokozi Yesu
Anipenda, anipenda
Anipenda Mwokozi Yesu
Anipenda mimi
[4]
Haya kujua yanipa raha
Kumwamini kuna furaha
Humfukuza mara shetani
Kwona yu nami Yesu pendoni
[chorus]
Anipenda Mwokozi Yesu
Anipenda, anipenda
Anipenda Mwokozi Yesu
Anipenda mimi
[5]
Sifa ni nyingi asifiwazo
Moja ni sana katika hizo
Wala siachi hata mbinguni
Kwimba " Yu nami Yesu pendoni "
[chorus]
Anipenda Mwokozi Yesu
Anipenda, anipenda
Anipenda Mwokozi Yesu
Anipenda mimi
Support Mysongbooks
Support us by joining the Buy Me A Coffee community and making a small donation, you can help us expand our library and ensure that music lovers everywhere can enjoy their favorite songs to the fullest. We're passionate about music, and we know you are too, so let's work together to keep the music alive.
Thank you for being a part of our community and supporting our mission to provide the best lyrics library on the internet.