Naomba
[Refrain]
Naomba Baba, mi naomba, mikono nimeinua
Nishike Baba, unifiche mikononi mwako
Nionyeshe Baba wema wako, unifanye chombo chako
Ninaomba, naomba, baba mi naomba
Sikudhani mimi nimekupa we huzuni kiasi hicho
Dhambi nyingi maombi hayatoki nisamehe Baba
Uchovu na uvivu umenijaza; moyoni sina amani
Naomba unipe raha msamaha uwashe taa
Popote niendapo, chochote nifanyacho, nifungue macho
Nipate kuona, na kuhisi, nipate upako wako
[Refrain]
Naomba Baba, mi naomba, mikono nimeinua
Nishike Baba, unifiche mikononi mwako
Nionyeshe Baba wema wako, unifanye chombo chako
Ninaomba, naomba, baba mi naomba
Sikudhani mimi nikiteleza, nakusulubu tena
Uchungu mwingi machozi yakutoka, nisamehe Baba
Unizibie ufa, nisijenge ukuta, Bwana umetukua
Naomba unipe raha msamaha, uwashe taa
Popote niendapo chochote nifanyacho, nifungue macho
Nipate kuona, na kuhisi, nipate upako wako
[Refrain]
Naomba Baba, mi naomba, mikono nimeinua
Nishike Baba, unifiche mikononi mwako
Nionyeshe Baba wema wako, unifanye chombo chako
Ninaomba, naomba, baba mi naomba
Support Mysongbooks
Support us by joining the Buy Me A Coffee community and making a small donation, you can help us expand our library and ensure that music lovers everywhere can enjoy their favorite songs to the fullest. We're passionate about music, and we know you are too, so let's work together to keep the music alive.
Thank you for being a part of our community and supporting our mission to provide the best lyrics library on the internet.
Buy us a coffee